IQNA

Swala ya jamaa yaruhusiwa katika Msikiti wa Makka

11:57 - October 18, 2020
Habari ID: 3473270
TEHRAN (IQNA) – Serikali ya Saudi Arabia imewaruhusu raia na wakaazi wa ufalme huo kuswali swala za jamaa za kila siku katika Msikiti Mtakatifu wa Makka (Al Masjid Al Haram ).

Kwa mujibu wa televisheni ya Saudia, hii itakuwa mara ya kwanza kwa swala za jamaa za kila siku kuswaliwa katika msikiti huo mtakatifu zaidi katika Uislamu baada ya kufungwa  kwa takribani miezi saba kutokana na janga la corona.

Mapema mwezi huu Saudia iliwaruhusu raia wake na wakaazi wan chi hiyo kutekeleza ibada ya Umrah mjini Makka na pia kufanya ziyara katika Msikiti wa Mtume SAW (Al-Masjid an-NabawI) katika mji wa Madina.

Idadi ya walioambukizwa corona nchini Saudia ni zaidi ya 342,000 huku waliopoteza maisha kutokana na ugonjwa huo wakiwa zaidi ya 5,100.

3929806

captcha