IQNA

Maeneo maalumu ya viziwi na wenye ulemavu wa macho yatengwa katika Msikiti wa Makka

20:39 - February 22, 2021
Habari ID: 3473673
TEHRAN (IQNA)- Maeneo maalumu ya swala yametengwa katika Msikiti Mtakatifu wa Makka (Al Masjid Al Haram ) kwa ajili ya walemavu.

Idara ya Usimamizi wa Misikiti Miwili Mitakatifu ya Makka na Madina imesema maeneo hayo ni maalumu kwa walemavu hasa viziwi na walemavu wa macho.

Idara hiyo imesema watu wenye mafunzo maalumu wamewekwa katika maeneo hayo kuwasaidia wanaofika katika eneo hilo la ibada.

Kati ya huduma zinazotolewa hapo ni kufasiri kwa lugha ya ishara na kutoa mafunzo ya qiraa na tafsiri ya Qur’ani Tukufu.

Katika kipindi hiki cha janga la Corona maeneo hayo yatakuwa yakisafishwa na dawa maalumu za kuua virusi.

3474057

captcha