IQNA

Mashindano ya Qur’ani ya watoto walemavu yafanyika Saudia

19:41 - April 26, 2021
Habari ID: 3473850
TEHRAN (IQNA)- Mashindano ya 25 ya Kuhifadhi Qur’ani Tukufu ya Mwanamfalme Sultan bin Salman maalumu watoto wenye ulemavu yamefanyika Saudi Arabia na washindi 34 kutunukiwa zawadi.

Mwanamfalme Sultan bin Salman bin Abdul Aziz, ambaye ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Watoto Walemavu, amewapongeza washindi.

Amesema mashindano hayo yameweza kutia fora kitaifa na kimataifa katika kipindi cha miaka 25 sasa. Halikadhalika amesema uzoefu wa huko nyuma utapelekea yaboreshwa zaidi katika siku za usoni huku akibainisha matumaini yake kuwa mwakani yatafanyika kwa  kushiriki katika ukumbi washindano baada ya kumalizika janga la corona.

Katibu mkuu wa mashindano hayo, Abdul Aziz bin Abdulrahman Al-Subaihin, amesema mashindano ya mwaka huu yalikuwa na washiriki  86 kutoka Saudia, Umoja wa Falme za Kiarabu na Bahrain.

/3474558

Kishikizo: walemavu saudia
captcha