Tamthilia za Ta'ziya hufanyika maeneo mbali mbali Iran katika miezi ya Muharram na Safar ili kuwabainishia watu yaliyojiri huko Karbala wakati Imam Hussein alipouawa shahidi tarehe 10 Muharram miaka 1382 iliyopita kulingana na kalenda ya Hijria. Katika tukio hilo moja kati ya vita mashuhuri katika historia ya Kiislamu na ya mwanadamu, vilitokea baina ya majeshi ya haki na batili katika ardhi ya Karbala huko Iraq.