IQNA

Haram Tukufu ya Hadhrat Abbas imepambwa wakati wa Idi za Sha’aban

TEHRAN (IQNA) – Kaburi tukufu (Haram) la Hadhrat Abbas (AS) huko Karbala, Iraq, lilipambwa kwa maua kabla ya hafla za furaha za mwezi wa Hijria Qamaria wa Sha’aban.

Siku ya 3, 4 na 5 ya Sha’aban (Februari 24, 25, na 26 mwaka huu) ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imam Hussein (AS), Hadhrat Abbas (AS) na Imam Sajjad (AS) mtawalia ambao ni katika Ahul Bayt wa Mtume Muhammad (SAW). Siku hizi ni maarufu kama Idi za Sha'aban.