Taarifa ya kituo hicho imesema mashindano hayo yalianza tarehe 7 katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani na yataendelea hadi siku ya mwisho ya mwezi huu.
Washiriki wanaulizwa maswali kupitia mtandao wa kijamii wa Telegram kila usiku na washindi wanatangazwa baadaye.
Mashindano hayo yanafanyika kila siku kuanzia saa moja usiku na washiriki wanapata fursa ya hadi saa kumi alasiri siku inayofuata kujibu maswali. Washindi wanapata zawadi kama vile kitabu, tasbihi, marashi, zulia la kuswalia n.k. Washiriki kutoka nje ya Sweden wanaweza kushiriki lakini wakishinda zawadi zao zinaweza kutumwa tu ndani ya Sweden.