IQNA

Jinai za Israel

UN: Rafah isishambuliwe, Wapalestina Gaza wanasubiri kusitisha mapigano

17:30 - May 02, 2024
Habari ID: 3478756
IQNA: Wakati kukiwa na ongezeko la wito wa kimataifa kwa Israel kujizuia na mashambulizi zaidi Gaza na ripoti za Mei Mosi za mashambulizi mengine mabaya, wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wamesisitiza kuhusu athari mbaya zinazoendelea za vita hiyo na haja ya kuhakikisha njia za kuaminika za usambazaji wa misaada kwa watu wanaohitaji kwa udi na uvumba zinapatikana.

UN: Rafah isishambuliwe, Wapalestina Gaza wanasubiri kusitisha mapigano

IQNA: Wakati kukiwa na ongezeko la wito wa kimataifa kwa Israel kujizuia na mashambulizi zaidi Gaza na ripoti za Mei Mosi za mashambulizi mengine mabaya, wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wamesisitiza kuhusu athari mbaya zinazoendelea za vita hiyo na haja ya kuhakikisha njia za kuaminika za usambazaji wa misaada kwa watu wanaohitaji kwa udi na uvumba zinapatikana.

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula Duniani WFP kupitia mkurugenzi wake wa eneo linalokaliwa la Palestina Matthew Hollingworth, limesema "Theluthi moja ya familia zote zinazoishi hapa zina watoto wa umri wa chini ya miaka mitano, hao ni watoto wengi sana.”

Akizungumza kutoka shule ya Deir Al Balah, inayoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA amesema watoto hawa wana mahitaji mengi “Wanachohitaji ni shule, maji safi na salama, utulivu zaidi,  na pia wanahitaji kurejea kwa maisha ya kawaida, "

Likiunga mkono wasiwasi huo shirika la UNRWA limegusia mashambulizi yanayoendelea likisema “kumekuwa na zaidi ya mashambulizi 360 kwenye vituo vyake tangu kuanza kwa vita. Mbali na makumi ya maelfu ya waathiriwa, miundombinu muhimu imeathiriwa pia, pamoja na kisima cha maji cha shirika hilo kilichoko katika jiji la Khan Younis.”

Na ili kukarabati chanzo hicho cha maji UNRWA inasema kunahitajika kuondoa tani za uchafu ikiwemo vilipuzi na vifaa vingie vya mabaki ya virta kama vilivyobainiwa na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya msaada wa kutegua mabomu UNMAS nav yote vinahitaji kuondolewa kwa usalama kipande kwa kipande,."

Shule ya UNRWA  ya Al Qastal iliyoko katikati mwa Ukanda wa Gaza sasa ni nyumbani kwa karibu familia 2,400 ambazo zimefurushwa na vita vya karibu miezi saba huko Gaza.

Bwana. Hollingworth  ameongeza kuwa "Watu wanatoka kote Ukanda wa Gaza, kuanzia mji wa Gaza wenyewe,mji jirani wa Khan Younis na kutoka katika vitongoji vyote tofauti ambako watu wameathiriwa kwa sababu ya vita,”

Kauli yake inakuja huku kukiwa na ripoti ambazo hazijathibitishwa kwamba watoto wawili wamekufa katika mashambulizi ya utawala haramu wa Israel Jumanne kwenye nyumba moja huko Rafah, na wengine kuuawa wakati ghorofa wanamoishi lilipopigwa na kombora katika mji wa Gaza.

Wakati wasiwasi mkubwa ukiendelea kuhusu uwezekano wa uvamizi wa Israel katika mji wa Rafah ambao Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres alionya Jumanne kwamba "Yatakuwa ni mashambulizi yasiyoweza kuvumilika" - afisa huyo wa WFP amebainisha kuwa mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa pamoja na washirika wengine wa kimataifa na wa ndani wamefanya kazi pamoja kwa mafanikio ili kutoa msaada wa kuokoa maisha hususani katika eneo la kaskazini.

Takwimu za hivi karibuni za mamlaka ya afya ya Gaza zinaonyesha kuwa Wapalestina wasiopungua 34,568 wameuawa na 77,765 wamejeruhiwa, wengi wakiwa ni wanawake na watoto katika vita vya mauaji ya kimbari vinavyoendeshwa na utawala haramu wa Israel kwa himaya ya Marekani dhidi ya Wapalestina huko Gaza tangu Oktoba 7.

3488160

 

Habari zinazohusiana
captcha