IQNA

Mtazamo

Msomi wa Lebanon: Shahidi Motahhari alipinga madai ya Wayahudi kuhusu umiliki wa Palestina

14:36 - May 03, 2024
Habari ID: 3478764
IQNA – Ustadh Shahidi Murtadha Motahhari, katika hotuba na maandishi yake, alipinga vikali upotoshaji wa historia kwamba eti ardhi ya Palestina ni milki ya Wayahudi.

Haya ni kwa mujibu wa profesa wa chuo kikuu cha Lebanon Talal al-Atrisi. Alisema hayo katika hotuba yake kwenye semina ya mtandaoni kuhusu ‘Palestine Katika Fikra za Shahidi Murtadha Motahhari’.

Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) iliandaa kongamano hilo la mtandaoni Jumatano asubuhi, kuadhimisha kumbukumbu ya kuuawa shahidi mwanazuoni huyo mkubwa wa Kiislamu.

Atrisi alisema kwamba Shahidi Motahhari alibainisha kwamba Waislamu walipoiteka Palestina, kulikuwa na Wakristo na si Wayahudi.

Pia alisema kwamba katika ramani zote za zamani, ardhi hiyo ilijulikana kama Palestina, ambayo inaonyesha kuwa haikuwa ya Wayahudi, Atrisi alisema.

Mwanazuoni huyo wa Lebanon aliendelea kusema kuwa, Shahidi Motahhari alikataa fikra ya kuwa Wayahudi ni taifa ili wapate haki ya kuikalia kwa mabavu Palestina na kuishi humo.

Shahidi Motahhari aliamini kwamba jaribio lolote la kuondoa utambulisho wa taifa la Palestina halingefanikiwa, aliendelea kusema.

Mwanafikra huyo mkubwa wa Kiirani alikuwa na mtazamo wa wazi na wa kistratijia kuhusu suala la Palestina na taifa la Palestina na alitetea uungaji mkono kwa Palestina katika wakati ambapo utawala wa kifalme wa Shah (dikteta aliyepinduliwa Iran kabla ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu) ulidumisha uhusiano mzuri sana na utawala haramu wa Israel, alisema.

Kwingineko katika maelezo yake, Atrisi alisema kwa kazi zake, Shahidi Motahhari aliacha urithi mkubwa katika nyanja za iitikadi na kijamii na katika kujibu nadharia zilizotaka kudhoofisha Uislamu.

Msomi wa Lebanon Hujjatul Islam Shafiq Jaradi, profesa wa chuo kikuu cha Iraq Sattar Qassim Abdullah, mwanafikra wa Bahrain Yaseen Fadhl al-Musawi, na Ali Motahhari, mwanae Shahidi Motahhari, pia walihutubia semina hiyo.

Murtadha Motahhari alikuwa mwanazuoni, mwanafalsafa na mhadhiri maarufu wa Kishia nchini Iran. Alikuwa mwanafunzi Allamah Tabatabai na Imam Khomeini na mwanzilishi mwenza wa Jumuiya ya Wanazuoni Wanamapambano. Mwanazuoni huyo aliuawa shahidi mwaka 1979.

Motahhari aliandika au kutoa mhadhara juu ya mada mbalimbali zinazohusiana na Uislamu, Iran, na historia, kama vile falsafa ya Kiislamu, teolojia, maadili, fiqhi, tafsiri ya Qur'ani, Sira ya Mtume Muhammad (SAW) na Maimamu (AS), na tukio la Ashura. . Pia alichambua masuala ya kisasa kama vile Umaksi, Umagharibi, haki za wanawake, na uamsho wa Kiislamu.

3488171

Kishikizo: palestina mayahudi
captcha