IQNA

Msomi: Uislamu unasisitiza kuhusu kulindwa haki za binadamu

17:20 - May 02, 2024
Habari ID: 3478755
IQNA – Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahl-ul-Bayt (AS) amesema Uislamu ni mtetezi wa kweli wa haki za binadamu zikiwemo za wanawake.

Ayatullah Reza Ramezani ambaye amesafiri hadi Brazil kushiriki katika kongamano lililopewa jina la “Uislamu, Dini ya Mazungumzo na Maisha”, aliyasema hayo katika hadhara ya wanawake wa Kiislamu kutoka nchi tofauti za Amerika ya Kusini.

Ameashiria kukua kwa ufeministi katika miongo kadhaa iliyopita na kusema kuwa matokeo yake ni kutumiwa wanawake kama chombo tu cha kufikia malengo jamii za Magharibi.

Mwanazuoni huyo wa Kiislamu ametoa wito kwa wanawake wa Kiislamu kusoma kuhusu haki za wanawake, kujifunza maneno ya kisheria katika nyanja hizo na wauelimishe ulimwengu kuwa Uislamu ndio dini pekee inayoweza kutetea haki za binadamu zikiwemo za wanawake.

Pia alitupilia mbali wazo kwamba nchi za Magharibi zimeanzisha mazungumzo ya haki za binadamu, akibainisha kwamba Imam Sajjad (AS), Imamu wa nne wa Kishia, aliandika Risalat al-Huquq (Waraka wa Haki) miaka 1,250 iliyopita.

Ayatullah Ramezani ameongeza kuwa maneno ya Mtukufu Mtume Muhammad (SAW0 na Imam Ali (AS) kuhusu wanawake yako wazi katika vitabu na yote yaliyomo yanaashiria jinsi Uislamu unavyozipa umuhimu haki za wanawake.

Wakati wa Jahilliya (zama kabla ya ujio wa Uislamu huko Uarabuni) na wakati ambapo wanawake walichukuliwa kuwa watu wasio na utambulisho wao wenyewe na kuwa na wasichana kulionekana kuwa chanzo cha aibu, Mtukufu Mtume (SAW) alitetea heshima, utambulisho na haki za wanawake, alisema.

Aidha amesisitiza usawa wa wanaume na wanawake katika Uislamu na kusema kuwa katika Uislamu nafasi zote za kiroho ambazo wanaume wanaweza kuzipata zinapatikana pia kwa wanawake.

Akaashiria Aya ya 13 ya Surah Al-Hujurat ya Qur'ani Tukufu na akakariri kwamba Uislamu unawachukulia wanaume na wanawake kuwa sawa.

Ayatullah Ramezani pia alibainisha kuwa baadhi ya wanawake wametambulishwa katika Qur'ani Tukufu kama vielelezo vya kuigwa kwa wanadamu wote.

Kwingineko katika hotuba yake, Ayatullah Ramezani amewataka washiriki wa mkutano huo kuchunguza mitazamo ya hayati muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Imam Khomeini (RA) na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyed Ali Khamenei kuhusu wanawake.

3488162

Habari zinazohusiana
captcha