Mpango huo, unaofanyika katika ua la eneo hilo takatifu, unaongozwa na maqari watatu wa Qur'ani Tukufu—Ammar al-Hilli, Karrar al-Mayahi, na Thamer al-Fartusi—.
Mpango huo umeandaliwa na jumba la kisayansi la Qur'ani Tukufu kwenye eneo hilo, Al-Kafeel iliripoti Jumatatu.
Wageni kwenye haram hiyo takatifu wanaweza kuhudhuria mikusanyiko hiyo kila siku saa tisa alasiri.
Zaidi ya hayo, vipindi hivi vinarushwa mubashara au moja kwa moja na Kituo cha Habari cha Al-Kafeel na hivyo kuwezesha hadhira pana kushiriki katika uzoefu wa kiroho.
Programu ya kila siku ya Khatm Qur'ani inalenga kuimarisha uhusiano na Qur'ani, kuhimiza ushirikiano wa mwaka mzima na aya zake na kutoa nafasi kwa wageni kujifunza na kutafakari Qur'ani Tukufu.
3488148