Kulingana na watumiaji wa mitandao ya kijamii, paa la chuma liliwekwa kwenye jengo hilo kama sehemu ya mipango ya upanuzi wa msikiti huo.
Hata hivyo, paa hilo halikuweza kustahimili uzito wa mvua hiyo na hivyo limeporomoka, na kuacha pengo kubwa katika dari ya msikiti huo.
Tangu Jumatano, mikoa kadhaa kote Saudi Arabia imeshuhudia mvua za wastani hadi kubwa. Wanafunzi kote Saudia waliambiwa wasome kwa njia ya intaneti kama tahadhari ya usalama.
Siku ya Jumatano, Kurugenzi Kuu ya Ulinzi wa Raia ilitoa maonyo makali ya hali ya hewa na maagizo ya usalama, ikiwataka watu kuchukua tahadhari na kubaki ndani ya nyumba wakati wa hali ya hewa ya dhoruba.
Karibu na hapo, radi kali zilipiga Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na hali ya mvua kali inataamiwa kuendelea Ijumaa.
3488178