Kile ambacho Quran inasema kuhusu nidhamu na utaratib kinaweza kugawanywa katika sehemu mbili: Takwini (inayohusiana na uumbaji) na Tashriei (inayohusiana na sheria). Katika kueleza utaratibu wa Takwini, Qur'ani Tukufu inarejelea mifano ya utaratibu unaotawala dunia na kuwaalika watu kuutafakari ili wajifunze kuhusu Aliyeumba utaratibu huu.
Kwa mfano, kuna marejeleo ya mpangilio sahihi angani, kama vile mwendo wa sayari katika mizunguko yao mahususi kwa mamilioni ya miaka. “ Haliwi jua kuufikia mwezi, wala usiku kuupita mchana. Na vyote vinaogelea katika njia zao (obiti).” (Aya ya 40 ya Surah Yaseen)
Kuna utaratibu na nidhamu ya ajabu katika uumbaji wa mbingu: “ Kwani hamwoni jinsi Mwenyezi Mungu alivyo ziumba mbingu saba kwa matabaka? (Aya ya 15 ya Surah Nuh)
Neno 'ulimwengu uliopangwa vizuri' ambalo lilianza kutumika katika karne ya 20 kwa hakika ni marejeo ya ukweli katika aya kama hizo za Qur'an, ukweli kwamba ulimwengu una mpangilio na muundo wa ajabu kwa ajili ya wanadamu kuishi katika ulimwengu huu.
Qur’an inataja baadhi tu ya mifano ya mpangilio huu mkubwa unaoeleweka kwa watu, ili waongoke kutoka kwenye utaratibu hadi kwa Aliyeuumba: “Je! Hawamtazami ngamia jinsi alivyo umbwa? Na mbingu jinsi ilivyo inuliwa? Na milima jinsi ilivyo thibitishwa? Na ardhi jinsi ilivyo tandazwa? (Aya ya 17-20 ya Surah Al-Ghashiyah)
Ukweli ni kwamba mpangilio sahihi na umakinifu unaoonekana katika kila kipengele cha uumbaji unadhihirisha hekima ya Mwenyezi Mungu na makusudio, ambayo msingi wake ni kwamba viumbe vyote vinaingia duniani kwa malengo fulani na kila jambo lina dhamira ya kutimiza. " Kwa hakika Sisi tumekiumba kila kitu kwa kipimo." (Aya ya 49 ya Surah Al-Qamar)
Kwa hiyo, katika ulimwengu, kila jambo limezingatiwa vizuri na kila kitu kiko mahali pake panapofaa, na hiyo ni dalili ya uumbaji wa ajabu ambao umetekelezwa na Mwenyezi Mungu mwenye hekima, ujuzi wote, na uwezo wote.
3488045