Shirika rasmi la habari la Bahrain limeripoti kuwa kuwa kamati za kielimu na ile ya majaji wa kongamano la wanakaligrafia bora wa Kiislamu zimekubali kazi 230 kati ya kazi zote 300 zilizowasilishwa.
Kongamano hilo limepangwa kufanyika yapata miezi miwili ijayo likisimamiwa na Kituo cha Qur'ani cha Mfalme Fahad mjini Madina na litawashirikisha wanakaligrafia wa Qur'ani kutoka ulimwengu wa Kiislamu.
Miongoni mwa malengo ya kongamano hilo ni kubainisha ujumbe muhimu wa wanakaligrafia wa Qur'ani Tukufu, kueleza uzoefu wao katika masuala ya Qur'ani, kuimarisha uhusiano baina ya wasanii hao na kuwaenzi. 747487