Kwa mujibu wa tovuti ya Mohet, kituo hicho kimesema kuwa Suratul Fatiha na sura 20 za mwisho za Qur'ani zimetarjumiwa na kufasiriwa kwa lugha ya ishara. Iwapo mradi huo utafanikiwa, utaendelezwa katika aya nyingine za Qur'ani Tukufu.
Muhammad bin Salem Shadid al Ufi mkurugenzi wa kituo hicho amesema kuna mpango wa kuzindua program za kompyuta kuhusu Qur'ani Tukufu maalumu kwa wanaotumia lugha ya ishara.
752440