IQNA

Mashindano ya Qur'ani na Hadithi maalumu kwa vijana wa Qatar yaanza

14:53 - March 01, 2011
Habari ID: 2088642
Duru ya 24 ya mashindano ya kitaifa ya Qur'ani na Hadithi maalumu kwa vijana wanachama wa vilabu vya michezo na vituo vya utamaduni vya Qatar yalianza nchini humo siku ya Jumapili tarehe 27 Februari.
Kwa mujibu wa gazeti la as-Sharq la Qatar mashindano hayo yameandaliwa na Idara ya Shughuli za Vijana ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Turathi ya nchi hiyo.
Mashindano hayo yanafanyika katika vitengo vinne vya hifdhi ya Qur'ani, sheria za usomaji na tajwidi ya Qur'ani, tafsiri na hadithi.
Akizungumzia suala hilo Jamal Faiz, mkuu wa kitengo cha shughuli za utamaduni cha Idara ya Shughuli za Vijana cha Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Turathi ya Qatar amesema vijana wote wanachama wa vilabu vya michezo na vituo vya vijana wanashiriki katika mashindano hayo. 755242
captcha