Kwa mujibu wa tovuti ya charentelibre, maonyesho hayo yatakuwa na anwani ya ‘Mohammad SAW, Rehma kwa Ulimengu’. Maonyesho hayo yametayarishwa na Jumuiya ya Mashirika ya Kiislamu Ufaransa.
Maonyesho hayo yatahudhuriwa na wanazuoni kutoka maeneo yote duniani ambao watajadili sira ya Mtume SAW.
Aidha kutakuwa na maonyesho ya sinema za Kiislamu, vitabu vya Kiislamu, taswira za maeneo matakatifu na vilevile mashindano ya qiraa na hifdhi ya Qur’ani maalumu kwa vijana na mabarobaro. Vilevile kutakuwa na mashindano ya mashairi yenye anwani ya ‘Mtume Muhammad SAW’.
Maonyesho hayo yataendelea hadi Disemba 19 na waandaaji wake wamesema Waislamu na wasiokuwa Waislamu wamealikwa kuhudhuria maonyesho hayo.
916481