IQNA

Utawala wa Israel waendelea kutengwa kimataifa kutokana na jinai zake Gaza

13:19 - October 05, 2025
Habari ID: 3481334
IQNA-Vita vya Ghaza na jinai nyingine zinazofanywa na utawala ghasibu wa Israel zimekabiliwa na msururu wa mashinikizo ya kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni ambayo yameufanya utawala huo ghasibu kuwa taifa linalochukiwa na kukataliwa duniani.

T-shirt Face Netanyahu Bloody Hand On Editorial Stock Photo - Stock Image |  Shutterstock Editorial

Katika ripoti iliyopewa jina la "From diplomacy to soccer, Israel is becoming a pariah on the global stage," kanali ya habari ya Marekani CNN imechunguza ongezeko la kutengwa utawala huo katika nyanja za kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na kimichezo na kusisitiza kwamba, vita na mgogoro wa kibinadamu unaoendelea huko Gaza umeongeza kasi ya utawala wa kizayuni ya kuwa utawala unaochukiwa.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kutengwa kwa utawala wa Israel kumeongezeka baada ya kutangazwa operesheni ya ardhini katika mji wa Gaza na shambulio lisilo la kawaida dhidi ya maafisa wa Hamas nchini Qatar. Kwa mujibu wa CNN, shutuma za kimataifa pia ziliongezeka baada ya kuchapishwa kwa ripoti ya jopo huru la Umoja wa Mataifa, ambapo shirika hilo lilikiri kwa mara ya kwanza kuwa utawala wa Israel ulifanya mauaji ya halaiki.

Mashinikizo ya kiuchumi na kibiashara

Kuhusiana na hilo, CNN iliripoti kuwa Umoja wa Ulaya, ukiwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa utawala wa Israel, umependekeza vikwazo vitakavyojumuisha kusitishwa sehemu ya makubaliano ya biashara huria. Nchi kadhaa za Magharibi tayari zimeweka vikwazo dhidi ya watu binafsi, walowezi wa Kizayuni, na mashirika yanayounga mkono vurugu katika Ukingo wa Magharibi.

Mfuko wa utajiri wa taifa wa Norway, mfuko mkubwa zaidi wa uwekezaji duniani umesimamisha baadhi ya vitega uchumi vyake katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu mwezi Agosti kutokana na mzozo wa kibinadamu huko Gaza. Aidha nchi kama vile Ufaransa, Italia, Uholanzi, Uhispania na Uingereza zimeuwekea utawala wa Israel vikwazo vya silaha kamili au sehemu.

NYC high schoolers stage walkout to protest Israel's war against Hamas |  The Times of Israel

Ripoti hiyo inasisitiza kuwa hata Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amelazimika kwa namnaa fulani "kutengwa" na ameonya kuwa, hali hii inaweza kuendelea kwa miaka. Ingawa baadaye alijaribu kupunguza maneno yake, CNN inaandika kwamba, maneno haya yanaonyesha wasiwasi halisi juu ya matokeo ya kiuchumi na kijeshi.

Vikwazo vya kiutamaduni na kisanaa

CNN inaandika kwamba, mwelekeo huu pia umeenea kwenye uwanja wa utamaduni na sanaa. Kanali za televisheni nchini Ireland, Uhispania na Uholanzi zimetangaza kwamba, zitasusia mashindano ya The Eurovision Song Contest 2026 iwapo utawala wa Israel utashiriki.

Huko Ubelgiji, maafisa wa tamasha la muziki walifuta tamasha moja la muziki likihusisha na uhusiano na "serikali ya kijinai ya Tel Aviv." Katika tasnia ya filamu, maelfu ya waigizaji na wakurugenzi wa Hollywood, akiwemo Olivia Colman, Emma Stone, na Andrew Garfield, wameahidi kutoshirikiana na taasisi za filamu za Israel.

Huge Rally Held in UK Capital against Israeli Siege, Palestinians'  Suffering in Gaza

Mashinikizo ya kimichezo dhidi ya utawala wa kizayuni wa Israel

Hali hii pia inaonekana katika michezo. Hatua ya mwisho ya mbio za baiskeli ilisitishwa kutokana na maandamano makubwa ya waungaji mkono wa Palestina, na wachezaji wa Israel walipigwa marufuku kushiriki katika mashindano ya sataranji (chess) chini ya bendera ya Israel nchini Uhispania. Pia kuna ripoti kwamba maafisa wa michezo wa Israel wana wasiwasi kuhusu uwezekano wa kufungiwa kushiriki mashindano ya soka ya Ulaya.

Ripoti hiyo ililinganisha hali ya sasa ya Israel na enzi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini. Ilan Baruch, balozi wa zamani wa Israel nchini Afrika Kusini, aliiambia CNN kwamba, mashinikizo ya kiuutamaduni na michezo yanaweza kuwa na athari sawa na vikwazo dhidi ya utawala wa kibaguzi.

Malalamiko ya ndani na harakati za kimataifa

CNN pia iliripoti kuwa maandamano ya ndani katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) dhidi ya vita na kuunga mkono usitishaji vita yanaendelea. Ulimwenguni, vuguvugu la Kususia, Kutenga na Kuweka Vikwazo dhidi ya Israel, linalojulikana kwa kifupi kama BDS, linapata uzingatiaji zaidi na kuungwa mkono, likijaribu kutoa mashinikizo yanayofanana na yale ya wakati wa enzi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.

Ripoti hiyo pia imebainisha kuwa uchunguzi wa Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji ya kimbari huko Gaza umeongeza umakini katika uchunguzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), ambayo hapo awali ilitoa waranti ya kukamatwa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, hatua ambayo imemfanya asiweze kusafiri katika sehemu nyingi za dunia.

Netanyahu hivi majuzi alizuiwa kupita katika anga za Ufaransa na Uhispania wakati akisafiri kwenda New York kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Licha ya kutengwa huko, CNN iliandika kwamba Marekani inasalia kuwa muungaji mkono muhimu zaidi wa utawala wa kizayuni wa Israel.

4308769

Habari zinazohusiana
captcha