Mchakato wa makabidhiano wa mateka wa Israel huko Gaza umeanza kutekelezwa leo kama sehemu ya makubaliano ya usitishaji vita yaliyofikiwa kati ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) na utawala wa Israel.
Hamas imechapisha orodha ya mateka wa Israel walio hai watakaoachiwa huru ambao imekuwa ikiwashikilia huko Gaza tangu kuanza kwa mauaji ya kimbari ya Israel Oktoba 7, 2023.
Mkabala wa ubadilishanaji huo wa mateka, Israel pia itawaachia huru wafungwa 250 na watu wengine 1,700 waliokuwa wakishikiliwa na utawala huo.
Mabasi yaliyokuwa yamebeba wafungwa wa Kipalestina yalianza kuelekea kwenye kivuko cha Karem Abu Salem, yakijiandaa kwa ajili ya kuwaachia huru wafungwa hao katika saa chache zijazo.
Hamas imesema kuwa imejiandaa kuliachia huru kundi la pili la mateka wa Israel ifikapo saa nne asubuhi kwa wakati wa Palestina. Utawala ghasibu wa Kizayuni pia unaazamia kuwaachia huru wafungwa wa Kipalestina wakati huo.
Mabadilishano haya ni sehemu ya hatua ya kwanza ya makubaliano ya kusitisha vita kati ya Hamas na Israel, yaliyofikiwa kwa usuluhishi wa Qatar, Misri na Uturuki.
3494987