Vitabu vya kufunza swala, kuhifadhi Qur'ani Tukufu na misingi ya dini vimeongoza katika orodha ya vitabu vinavyouzwa kwa wingi katika maonyesho ya kimataifa ya vitabu mjini Dakar, Senegal.
Maafisa wa Maonyesho ya 13 ya Kimataifa ya Vitabu ya Dakar wameripoti kuwa vitabu vinavyohusiana na Uislamu, kuvumiliana na kuishi kwa pamoja wafuasi wa madhehebu mbalimbali za Kiislamu vimewavutia zaidi wanunuzi katika maonyesho hayo.
Ripoti zinasema vitabu vinavyohusu 'Maisha ya Nabii Muhammad (saw),' 'Nguzo za Swala na Udhuu Sahihi' na 'Umoja Baina ya Waislamu katika Nchi Mbalimbali' vimeuzwa kwa wingi katika maonyesho hayo ya vitabu.
Maonyesho ya Kimataifa a 13 ya Vitabu mjini Dakar yalimaliza kazi zake Alkhamisi iliyopita. 921290