IQNA

Mnada wa kazi za sanaa ya Kiislamu kufanyika Ufaransa

12:19 - January 05, 2012
Habari ID: 2251692
Taasisi ya mnada ya Artcurial ya Ufaransa tarehe 9 Februari itanadi kazi za sanaa ya Kiislamu katika Hoteli ya Marcel Dassault mjini Paris.
Tovuti ya 'Ama' imetangaza kuwa mnada huo unajumuisha sehemu mbili kuu za kazi za sanaa ya Mashariki na athari za Kiislamu.
Sehemu muhimu zaidi ya mnada huo ni ile itakayouza kurasa zenye thamani kubwa za Qur'ani Tukufu zilizoandikwa kwa hati za Kufi. Kurasa hizo ziliandikwa katika karne ya 10. Kurasa hizo zinakadiriwa kuwa zina thamani ya kati ya yuro elfu 18 hadi 25. 928977

captcha