IQNA

Jildi zaidi za Insaiklopidia ya Kiislamu kuchapishwa Iran

16:52 - January 17, 2012
Habari ID: 2258100
Jildi ya 19 ya Insaiklopidia ya Kiislamu kwa lugha ya Kifarsi itachapishwa hivi karibuni nchini Iran, amesema mkuu wa Kituo cha Insaiklopidia Kubwa ya Kiislamu.
Sayyid Kazem Mousavi Bojnourdi amemwambia mwandishi wa IQNA kuwa jildi ya tatu ya Kiingereza, ya nane ya Kiarabu na ya 19 ya Kifarsi ziko katika mkondo wa mwisho wa kuchapishwa katika taasisi hiyo.
Aidha ameashiria insaiklopidia mpya yenye jidli 30 kuhusu Iran na kuongeza kuwa tayari jildi ya nne imetayarishwa. Amesema mjumuiko huu mpya una makala kuhusu Iran na ulimwengu wa Kiislamu.
Mousavi amesema pia kwamba kuna mpango wa kuchapisha insaiklopidia kuhusu ngano za kale za Iran katika mjumuiko wa jildi 10 zenye maudhui 3000.
‘Kutayarisha insaiklopidia yenye jildi 8 kuhusu Ghuba ya Uajemi na vilevile jildi 14 kuhusu historia kamili ya Iran ni kati ya miradi ya hapo baadaye ya taasisi hii’, ameongeza.
935038
captcha