Gavana wa Najaf Adnan Al Zarfi ameongeza kuwa makongamano 10 yatafanyika mjini humo katika fremu ya kutangazwa Najafa kuwa 'Mji Mkuu wa Utamaduni wa Kiislamu mwaka 2012'.
Ameyataja baadhi ya makongamano hayo kuwa ni pamoja na 'Fiqhi ya Kiislamu', 'Historia ya Kiislamu' na Kukurubisha Madhehebu ya Kiislamu'.
Mkoa wa Salahuddin nchini Iran pia umetangaza kuwa uko tayari kushirikiana na Najaf katika kuandaa makongamano hayo.
Qassam Kalaf mkuu wa masuala ya utamaduni na sanaa katika mkoa huo amesema, 'kuna programu 15 tafauti ikiwa ni pamoja na maonyesho ya vitabu na maonyesho ya kaligrafia za kiarabu. Ameongeza kuwa malenga mashuhuri wa Iraq wataenziwa.
936589