IQNA

Kongamano la ‘Mwamko wa Kiislamu na Sinema’ kufanyika Iran

16:13 - January 28, 2012
Habari ID: 2262898
Wawakilishi kutoka nchi 9 watashiriki katika kongamano la ‘Mwamko wa Kiislamu na Sinema’ ambalo litafanyika katika Ukumbi wa Mnara wa Milad mjini Tehran Februari 5.
Kongamano hilo litajadili athari za sinema katika mwamko unaoshuhudiwa katika nchi za Kiarabu. Natija ya kongamano hilo itawasilishwa katika sherehe za kufunga Tamasha ya Kimataifa ya Fajr ya Filamu itakayofanyika Tehran.
Wataalamu 30 na wazungumzaji kutoka Kuwait, Misri, Algeria, Tunisia, Uturuki, Iraq, Yemen, Morocco na Uingereza pamoja na wanadiplomasia wa nchi kadhaa pia watashiriki.
Katibu wa kongamano la ‘Mwamko wa Kiislamu na Sinema’ ni Mohammad Khazaee.
Awamu ya 30 ya Tamasha ya Kimataifa ya Fajr ya Filamu itaanza Februari Mosi mjini Tehran. 940645
captcha