IQNA

Sayyid Nasrullah akosoa nchi za Kiarabu kwa kuchochea machafuko Syria

15:01 - February 26, 2012
Habari ID: 2280488
Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amezilaumu baadhi ya nchi za Kiarabu kwa kuchochea machafuko nchini Syria na kuzuia kupatikana suluhisho la kidiplomasia la kutatua machafuko hayo.
Sayyid Hassan Nasrullah amesema, baadhi ya nchi za Kiarabu zinayapa silaha na kuyaunga mkono makundi ya kigaidi yanayopigana dhidi ya serikali ya Rais Bashar al Assad wa Syria, suala ambalo linawazuia wapinzani kuingia katika mazungumzo ya kusaka amani na serikali.
Aidha Sayyid Nasrullah amezilamu baadhi ya nchi kwa kuyapa silaha makundi ya kigaidi ya Syria ili yavuruge utulivu wa nchi hiyo.
Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema, Marekani na nchi za Magharibi hazitaki mgogoro wa Syria utatuliwe kwa amani bali madola hayo yanajaribu kuzusha vita vya ndani nchini humo.
Sayyid Nasrullah pia ameashiria hatua ya wanajeshi vamizi wa Marekani kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu na kusikitika kuwa Waafghani wanaolalamikia kitendo hicho wanapigwa risasi. Amesema ni tabia ya Waisraeli katika historia kuwavunjia heshima Mitume wa Mwenyezi Mungu.
Katibu MKuu wa Hizbullah ameashiria kuenea makundi ya Takfiri na kusema kuwa makundi hayo yanapata uungaji mkono wa mashirika ya kijasusi ya Marekani na utawala wa Kizayuni. Amesema kuna haja ya nchi za eneo la Mashariki ya Kati kuchukua tahadhari ili kukabiliana na njama za Wazayuni
959405
captcha