Kwa mujibu wa Shirika la Iran la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu ICRO, semina hiyo itafanyika kwa mnasaba wa Wiki ya Utamaduni wa Iran nchini Indonesia kuanzia Machi 7-8.
Kikao hicho kinatazamiwa kuhudhuriwa na wasomi kutoka Iran, Indonesia, Malaysia na Thailand. Kati ya programu zingine za Wiki ya Utamaduni ya Iran ni maonyesho ya sinema, 'Usiku wa Utamaduni wa Iran', kikao cha kwanza cha pamoja cha tume ya utamaduni ya Iran na Indonesia. Aidha kutakuwa na vikao vya wasomi wa kidini na kiutamaduni wa Iran na Indonesia.
Hafla ya 'Wiki ya Utamaduni' ya Iran nchini Indonesia pia itahudhuriwa na Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Iran Dr. Sayyed Mohammad Hosseini.
963213