Tovuti ya Siasat imeripoti kuwa msanii huyo wa India amendika na kuchora aya za Qur'ani Tukufu katika zaidi ya misikiti 100 kwenye miji ya Hyderabad, Iskanderabad na kadhalika. Msanii huyo ameutumia umahiri wake katika sanaa ya kaligrafia kuandika aya za Qur'ani na dua za Kiislamu katika kuta na mihrabu nyingi za misikiti.
Miongoni mwa kazi muhimu za Anil Kumar Chauhan ni bango kubwa la maandishi ya aya za Suratu Yasin lililoko kwenye Chuo Kikuu cha Nizamiya nchini India.
Kazi nyingine za thamani za msanii huyo ni maandishi ya majina ya Mwenyezi Mungu (Asmaul Husna) na pia jina la Mtume Mtukufu Muhammad (saw). Kwa kawaida Anil Kumar huwa haombi ujira wa fedha kwa ajili ya kazi za kuchora aya za Qur'ani na maandishi mengine ya Kiislamu na hutosheka na chochote anachopewa mkabala wa kazi zake.
Msanii Anil Kumar Chauhan hutia udhuu kabla ya kuandika aya za Qur'ani Tukufu. 990401