Maonyesho hayo ya siku nne yameandaliwa na taasisi ya De Minaret International na yatafanyika kuanzia Jumamosi Mei 5-8.
Katika taarifa ya mkurugenzi wa taasisi hiyo Malam Saheed Abdur-Rauf, maonyesho hayo yanafanyika chini ya anwani ya: "Uislamu, Dini Iliyofahamiva visivyo" na yatafunguliwa na waziri wa zamani Dr. Aliyu Modibo.
Inatazamiwa kuwa Prof. Nuhu Yakubu, aliyekuwa naibu kansela wa Chuo Kikuu cha Abuja pia atahutubia kikao hicho.
De Minaret International ni taasisi isiyo ya kiserikali ambayo inajihusisha na ustawishaji utamaduni wa kusoma vitabu miongoni mwa Waislamu.
Karibu anwani 65,000 za vitabu kuhusu Uislamu, tafsiri za Qur'ani, hadithi, fiqhi ya Kiislamu, uchumi, siasa, jamii na watoto zinaonyeshwa katika maonyeshi hayo.
Maonyesho sawa na hayo yalifanyika Abuja mwaka 2011.
998833