IQNA

Kongamano la 'Uislamu na Jamii' kufanyika Iran

19:28 - May 02, 2012
Habari ID: 2317217
Kongamano la kila miaka miwili la Iran na Malaysia kuhusu Uislamu litafanyika mjini Tehran mwaka huu chini ya anwani ya, 'Uadilifu katika Uislamu'.
Kongamano hilo litakalofanyika Desemba 15-16 mwaka 2012 litawakutanisha pamoja watafiti, wasomi na wanafunzi wa vyuo vikuu ili waweze kubadilishana uzoefu, fikra mpya na natija ya utafiti kuhusu mtazamo wa Uislamu katika masuala ya uadilifu.
Maudhui zitakazojadiliwa ni pamoja na masuala ya intaneti na changamoto zake, masuala ya wanawake, uhusiano wa kimataifa, uandishi habari, sheria, mawasiliano na saikolojia.
Kongamano hilo limeandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kijamii na Utamaduni ya Iran, Wizara ya Sayansi, Utafiti na Teknolojia ya Iran na Chuo Kikuu cha Kebangsaan cha Malaysia.
Maelezo zaidi kuhusu kongamano hili yako katika tovuti ya www.imisc.org.
998734

captcha