IQNA

Wanaakiolojia wagundua kasri ya kale zaidi ya Kiislamu Iran

17:10 - May 10, 2012
Habari ID: 2322504
Wanaakiolojia wamefanikiwa kuchimbua kasri ya kale zaidi ya Kiislamu Iran walipokuwa wakifukua mji wa kale wa Estakhr katika mkoa wa Fars.
Akizungumza na IQNA, Mahmoud Mireskandari Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kiakiolojia katika Shirika la Turathi na Utalii Iran (ICHTO) amesema, 'jengo hili limegunduliwa katika ufukuaji wa pamoja na wanaakiolojia wa Italia na linaaminika kuwa lilijengwa kati ya karne za 14-15 Miladia.'
Ameongeza kuwa, 'Jengo hili lina kasri kubwa ambayo wakati moja ilikuwa makao makuu ya serikali.'
Amesema timu hiyo itaendelea na ufukuaji katika eneo hilo ili kupata maelezo kamili ya jengo hilo la kihistoria.
Estakhr ni mji wa kale ambao uko kilomita tano kaskazini mwa Persepolis ambao ulikuwa mji uliostawi katika zama za Wahaemeni waliotawala Iran mwaka 550-330 Kabla ya Miladia.
Kuna majengo mengi ya kale nchini Iran kabla na baada ya Uislamu. Ubora katika usanifu majengo wa Iran wa baada ya kudhihiri Uislamu katika ardhi hii ni jambo linaloashiria namna Wairani walivyoukumbatia Uislamu katika nyanja zake.
1004048
captcha