IQNA

Masomo ya misingi ya Kiislamu yatolewa kwa polisi ya Russia

12:01 - May 28, 2012
Habari ID: 2335925
Kwa mara ya kwanza polisi ya Russia imefundishwa misingi ya mafunzo ya Kiislamu. Kikao cha kwanza kwa masomo hayo kilifanyika siku ya Ijumaa katika mkoa wa Nizhny Novgorod ambapo polisi wapatao 60 walishiriki.
Kwa mujibu wa idara inayoshughulikia masuala ya kidini na Kiislamu katika mkoa huo, masomo hayo ya misingi ya mafundisho ya Kiislamu yanahusiana na historia pamoja na utamaduni wa Kiislamu. Masomo hayo yalitolewa na Abdul Bari Muslimov, naibu mkuu wa idara iliyotajwa. Maafisa wa polisi katika mkoa huo wameshukuru sana kwa juhudi kubwa alizofanya katika kufanikisha suala hilo kwa maslahi ya polisi ya mkoa huo. Masomo kama hayo yamepangwa kufanyika katika idara za polisi katika mikoa mingine ya Russia. 1017973
captcha