Kwa mujibu wa tovuti ya Pakistan Today, maonyesho hayo yameandaliwa na Kundi la Sanaa na Usanifu Majengo la chuo kikuu hicho. Zaidi ya athari 80 za sanaa inayohusiana na ramani, uchoraji na kaligrafia ya Kiislamu zimeonyeshwa na wanachuo wa kike wa chuo hicho katika maonyesho hayo. Kuhusu suala hilo, N.B Jumani, mkuu wa Chuo cha Elimu Jamii ya chuo hicho cha kimataifa amesema kwamba kaligrafia ni sehemu muhimu ya utamaduni na ustaarabu wa Kiislamu. Amewashukuru wanachuo wa kike wa Kiislamu walioshiriki kwenye maonyesho hayo na kusema kuwa suala hilo lina nafasi muhimu katika kunyanyua kiwango cha sanaa na usanifu majengo wa Kiislamu. Maonyesho hayo yamesifiwa na kukaribishwa na wachoraji pamoja na wahadhiri mashuhuri wa sanaa ya Kiislamu nchini Pakistan. 1020315