IQNA

Misikiti ya kihistoria ya utawala wa Othmania nchini Albania kukarabatiwa

11:58 - June 06, 2012
Habari ID: 2341016
Msikiti ya kihistoria ya kipindi cha utawala wa Othmania katika Jamhuri ya Albania imepangwa kukarabatiwa na Wakala wa Ushirikiano na Uratibu wa Uturuki kwa gharama ya euro milioni 4.
Akizungumzia suala hilo Yahya Gulsun, mkuu wa wakala huo tawi la Tirana mji mkuu wa Albania amesema kwamba misikiti hiyo ya kihistoria haipaswi kutazamwa kama turathi za kiutamaduni za nchi hiyo tu bali kama urithi wa kiutamaduni wa wanadamu wote duniani. Ameelezea matumaini kwamba misikiti mingine ya kale inayohitajia ukarabati pia itaongezwa kwewnye orodha ya misikiti ya kihistoria inayopaswa kukarabatiwa. 1022828
captcha