IQNA

Viongozi wa Kidini duniani wakutana Baku, wasisitiza kuhusu vita dhidi ya ugaidi

10:23 - November 18, 2019
Habari ID: 3472220
TEHRAN (IQNA) – Washiriki katika Mkutano wa Pili wa Viongozi wa Kidini Duniani umefanyika huko Baki katika Jamhuri ya Azerbaijan ambapo washiriki wamesisitiza kuhusu ulazima wa kuheshimu uwepo wa dini mbali mbali sambamba na kuendeleza vita dhidi ya ugaidi.

Kongamano hilo la siku mbili lilianza Novemba 14 na kuwaleta pamoja viongozi wa kidini pamoja na wasomi na wanasiasa kutoka nchi mbali mbali na pia wawakilishi wa taasisi za kimataifa.

Taarifa ya mwisho ya kikao hicho imetoa wito kwa Umoja wa Mataifa pamoja na asasi za kieneo na kimataifa kuchukua hatua za kuhakikisha kuwa kuna maelewano na ushirikiano baina ya dini na staarabu mbali mbali. Aidha wametoa wito wa kuwepo mikakati ya kuwazuia magaidi kutumia matukufu ya dini katika kufikia malengo yao haramu.

Mkutano huo uliofunguliwa rasmi na Rais  Ilham Aliyev wa Jamhuri ya Azerbaijan ulikuwa na wawakilishi kutoka nchi 70 kutoka mabara yote matao ya dunia.

Miongoni mwa wazungumzaji katika mkutano huo walikuwa ni Mwenyekiti wa Ofisi ya Waislamu katika eneo la Caucasus Sheikhulislam Allahshukur Pashazade, kiongozi wa Kikristo wa Russia Patriarch Kirill na Dkt. Ibrahimi Torkman, Mkuu wa Shirika la Iran la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu (ICRO).

3857479

captcha