IQNA

Harakati za Qur'ani

Qari wa Misri aliyesafiri katika Nchi 100 kwa ajili ya kusoma Qur'ani

21:30 - May 06, 2024
Habari ID: 3478782
IQNA - Mohamed Mahmoud Tiblawi alikuwa qari mashuhuri nchini Misri ambaye aliwahi kuwa rais wa Jumuiya ya Wasomaji na Wahifadhi wa Qur'ani nchini humo kwa miaka kadhaa.

Jana, Mei 5, iliadhimisha mwaka wa 4 wa kifo cha qari huyu maarufu wa Qur'ani wa Misri.
Tiblawi alizaliwa Novemba 14, 1934, katika kijiji cha Giza. Baba yake alimpeleka Maktab (shule ya jadi ya Qur'ani) ya kijiji hicho kujifunza Qur'ani akiwa na umri wa miaka minne.
Alijifunza usomaji wa Qur'ani na kisha akahifadhi Qur'ani nzima akiwa na miaka 14. Tiblawi alianza kusoma Quran katika vipindi tofauti na punde akaalikwa kwenye Redio ya Qur'ani. Alisafiri katika takriban nchi 100 kwa ajili ya kusoma Qur'ani Tukufu kama mwakilishi wa wizara ya wakfu ya  Misri au Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar.
Pia aliwahi kuwa mjumbe wa jopo la majaji  katika mashindano mbalimbali ya kimataifa ya Qur'ani.
Alipokea tuzo ya juu wa serikali ya Lebanon kwa juhudi zake za kuitumikia Qur'ani Tukufu.
Tiblawi aliaga dunia mnamo Mei 5, 2020, akiwa na umri wa miaka 86 na baada ya kutumikia Qur'ani Tukufu kwa miongo kadhaa.
Hapa chini ni klipu za qiraa yake ya Aya za 85 hadi 88 za Surah Al-Anbiya na 84 hadi 86 za Surah Yunus.

 

 

3488217

Habari zinazohusiana
Kishikizo: qurani tukufu qari misri
captcha