Hujjatul Islam Abdul Fattah Navab, mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Masuala ya Hija na Ziyara za Kidini ameyasema hayo jijini Tehran alipokuwa akiwahutubia maelfu ya Wairani mjini Tehran waliokusanyika katika Uwanja wa Azadi siku ya Ijumaa kwa ajili ya kupata mafunzo ya ibada ya Hija.
"Chochote tulichonacho kinatokana na Qur'ani Tukufu na Ahlul-Bayt (AS). Ipe kipaumbele Qur'ani Tukufu na uwe na uwelewa wa Wahy wa Mwenyezi Mungu katika Hija," alisema.
Katika miaka ya hivi karibuni, baadhi ya Mahujaji waliweza kuhifadhi Juzuu ya 30 ya Qur'ani wakati wa ibada ya Hija na baadhi ya wengine waliweza kuhitimisha Qur'ani wakati wa ibada ya Hija, alisema. "Hii ni hatua yenye thamani sana", alibaini afisa huyo wa Hija wa Iran.
Mwaka huu zaidi ya Wairani 83,000 wanatazamiwa kuelekea Saudi Arabia katika wiki zijazo kwa ajili ya Ibada ya Hija.
Navvab pia alisisitiza haja ya kuwepo huruma na umoja baina Mahujaji. "Kuna wale wanaotaka kuzusha mifarakano ndani ya Umma wa Kiislamu."
"Kwa hiyo, ni muhimu kwa jumuiya ya Kiislamu kukabiliana na mbinu hizi za mgawanyiko kwa kukuza uelewa na mshikamano," Hujjatul Islam Navab alisema.
Kwingineko, amewataka mahujaji wa Hijja kuwaunga mkono watu wanaodhulumiwa wa Gaza, ambako zaidi ya Wapalestina 35,000 wameuawa na uvamizi wa Israel tangu Oktoba.
Inatia moyo kuona hata wanafunzi kutoka nchi za Magharibi wakitetea watu wa Gaza, alisema, akiashiria maandamano ya wanafunzi na wahadhiri katika vyuo vikuu kote Marekani na nchi zingine kadhaa kuunga mkono Gaza.
"Ninawahimiza Mahujaji kujitolea Tawaf yao kwa ajili ya mashahidi wa Gaza, kwa wakazi wanaodhulumiwa wa eneo hilo, na kwa watoto ambao wameteseka," Hujjatul Islam Navab alisema.
3488199