IQNA

Jinai za Israel

Uharibifu uliosababishwa na Israel Gaza haujawahi kuonekana tangu Vita vya Pili vya Dunia

18:47 - May 04, 2024
Habari ID: 3478771
IQNA-Afisa wa Umoja wa Mataifa anasema uharibifu uliosababishwa na vita vya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza haujawahi kuonekana tangu Vita vya Pili vya Dunia, huku akikadiria kuwa ujenzi mpya wa eneo hilo la Palestina unaweza kuchukua miaka 80 na kugharimu hadi dola bilioni 40.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika mji mkuu wa Jordan Amman siku ya Alhamisi, Abdallah al-Dardari, msaidizi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na mkurugenzi wa ofisi ya kanda ya Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa mataifa ya Kiarabu, ameongeza kuwa uvamizi wa Israel umeangamiza kabisa au kwa kiasi asilimia 72 ya majengo yote ya makazi huko Gaza.

Pia amekadiria kuwa mashambulizi ya Israel yameacha tani milioni 37 za vifusi kote Gaza, akionya kwamba vifusi vinaongezeka kila siku na kukaribia tani milioni 40.

Dardari amesema kuwa ujenzi wa Ukanda wa Gaza kupitia mchakato wa kawaida unaweza kuchukua miongo kadhaa.

Hapo awali, Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa ulitoa tathmini, na kubainisha kwamba Gaza itahitaji "takriban miaka 80 kurejesha nyumba zilizoharibiwa katika hali ya kawaida."

Utawala katili wa Israel umekuwa ukidondosha mabomu kila siku katika Ukanda wa Gaza na Umoja wa Mataifa unasema zoezi la kutegua mabomu ambayo hayajalipuka eneo hilo hadi sasa linaweza kuchukua muda wa miaka 14.

Afisa Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Huduma ya Uteguzi wa Mabomu UNMAS Pehr Lodhammar ameyabainisha hayo na kuongeza kuwa vita huko Gaza vimeacha ardhini takriban tani milioni 37 za mabomu.

Utawala haramu wa Israel ulianzisha vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza Oktoba 7 mwaka jana na hadi sasa utawala huo katili umeua shahidi zaidi ya Wapalestina 34,596   na kujeruhi wengine 77,800, wengi wakiwa ni wanawake na watoto.

3488185

Habari zinazohusiana
captcha