IQNA

Nidhamu katika Qur’ani/ 10

Swalah huleta nidhamu katika maisha ya Muumini

23:28 - May 07, 2024
Habari ID: 3478788
IQNA - Msingi wa utaratibu katika maisha ya Muislamu ni kumwabudu Mwenyezi Mungu na ndiyo maana kuswali swala tano za kila siku humsaidia mja kupanga shughuli zake za kila siku.

Moja ya mambo yanayochangia nidhamu  ni taratibu za kidini ambazo zina muda maalum wa kufanywa. Kwa mfano, Qur’ani Tukufu inabainisha kuwa mwezi mtukufu wa Ramadhani ni kwa ajili ya kufunga. Ina mwanzo na mwisho maalum, ambayo hutegemea mwezi mwandamu. (Aya ya 187 ya Surah Al-Baqarah)

Pia kuna nyakati mahususi za kufanya ibada kama vile Swalah: “Salini sala yenu jua linapopungua mpaka giza la usiku na pia alfajiri. Hakika alfajiri inashuhudiwa (na Malaika wa usiku na mchana). (Aya ya 78 ya Suratul Israa)

Imam Ali (AS) alimwambia Muhammad bin Abi Bakr: “Sali swala kwa wakati uliowekwa. Usiswali mapema kwa ajili ya burudani (iliyopo) wala usicheleweshe kwa sababu ya kujishughulisha. Kumbuka kwamba kila kitendo chako kinategemea swala yako.” Kwa hiyo kuswali swala tano za kila siku kunamsaidia mtu kupanga shughuli zake za kila siku. Kujifunza namna ya kutekeleza Swalah na yale yanayopaswa kusomwa moja baada ya jingine wakati wa Swalah hupelekea utulivu katika akili.

Kushiriki swala ya jamaa pia ni zoezi ambalo hutegemea nidhamu na utaratibu maalumu. Mtukufu Mtume (SAW.) amesema kuhusu swala za jamaa: Enyi watu! (Katika Swalah za jamaa) timizeni safu zenu na mweke mabega yenu karibu, jaza mapengo na wala msipingane ….”

Waumini pia wana nidhamu na utaratibu katika mambo ya kijamii na hufanya shughuli zao zote, hasa katika mambo muhimu na yenye maamuzi, kwa idhini ya kiongozi wa jamii. Iwapo mtu atashindwa kufanya hivyo, hatahesabiwa kuwa miongoni mwa waumini wa kweli: “Hakika Waumini ni wale wanaomwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na ambao wanapokusanywa pamoja naye katika jambo la kawaida hawaondoki mpaka wamuombe ruhusa yake.” (Aya ya 62 ya Surat An-Nur).

3488142

Kishikizo: qurani tukufu swala
captcha