IQNA

Wakristo waadhimisha Paska katika zama za corona

Wakristo katika maeneo mbali mbali duniani wanaadhmisha sikukuu ya Pasaka tafauti na miaka iliyopita kutokana na kuenea janga la ugonjwa wa corona au COVID-19 duniani.

Pasaka ya Kikristo, ambayo inapatikana katika moja ya Jumapili za Machi au Aprili, ni sikukuu ya kufanya ukumbusho wa kile Wakristo wanachoamini  kuwa ni kufufuka kwake Nabii Issa AS siku ya tatu baada ya kusulubiwa, kufa na kuzikwa kwake.