TEHRAN (IQNA) – Katika hafla adhimu iliyofanyika katika Ukumbi wa Hekmat, ndani ya Maktaba ya Kitaifa na Nyaraka za Iran, mnamo tarehe 29 Julai 2026, ulimwengu ulishuhudia kuzinduliwa kwa Msahafu wa Zaferani.
Nakala hii ya Qur'ani inatajwa kuwa ya kale zaidi inayojumuisha tafsiri ya Kifarsi; tukio hili ni kielelezo kingine cha mchango mkubwa wa ustaarabu wa Kiislamu wa Uajemi katika kuhifadhi na kueneza nuru ya Uislamu.