IQNA

Maelfu ya Mazuwaru wa Arbaeen Wapita Mkoa wa Ilam Kuelekea Iraq

IQNA – Huku wimbi la ziara tukufu ya Arbaeen likiwa limeanza na mamilioni ya wapenzi maashiki wa Ahlul-Bayt wa Mtume Muhammad (SAW) kutoka Iran wakielekea mji mtukufu wa Karbala, mkoa wa Ilam, ambao ni moja a njia kuu na muhimu zaidi kwa ajili ya mazuwaru, unapokea na kuhudumia maelfu ya mazuwaru wa ndani na nje ya nchi kila siku. Katika njia hiyo, Mawkib (kituo cha huduma bila malipo) cha “Wapenzi wa Amir al-Mu’mineen (AS)” kinaendelea kutoa huduma kwa mazuwaru hao usiku na mchana bila kupumzika.