IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Iran lilisimama kidete mbele ya madola ya Mashariki, Magharibi na tawala tegemezi, na kuibuka mshindi

18:58 - September 21, 2020
Habari ID: 3473189
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amezungumzia ushindi mkubwa na wa wazi wa taifa la Iran katika Vita vya Kujitetea Kutakatifu na kusema kuwa: Kujitetea kutakatifu ni sehemu ya utambulisho wa kitaifa wa Iran.

Ayatullah Ali Khamenei ameyasema hayo mapema leo kupitia njia ya video katika sherehe ya kuwaenzi wakongwe wa vita vya Kujitetea Kutakatifu vilivyoanzishwa na Saddam Hussein dhidi ya Iran na kuongeza kuwa: Katika vita hivyo taifa la Iran lilisimama kidete mbele ya madola ya Mashariki na Magharibi na nchi tegemezi, na kuibuka na ushindi.

Ayatullah Khamenei amesema kuwa, Saddam Hussein mpenda jaha alikuwa wenzo wa madola makubwa hususan Marekani na kuongeza kuwa: Upande asili wa vita hivyo dhidi ya taifa la Iran, yaani Marekani iliyopata kichapo kutokana na ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, madola yaliyokuwa na wasiwasi kutokana na kujitokeza utambulisho mpya wa Kiislamu na Kiirani katika eneo la Magharibi mwa Asia, NATO na nchi za Ulaya Mashariki na Magharibi, zilimhamasisha Saddam kuishambulia Iran ili kutokomeza kabisa utawala na Mapinduzi ya Kiislamu.

Amesema kuwa, lengo la maadui katika kuanzisha vita hivyo lilikuwa kuuondoa madarakani utawala wa Kiislamu hapa nchini, kuidhibiti tena Iran na kuigawa; lakini hawakuweza kukalia kwa mabavu hata shibri moja ya ardhi ya Iran wala hawakuweza kuirudisha nyuma Jamhuri ya Kiislamu na taifa la Iran hata hatua moja.

Ayatullah Khamenei ameashiria nyaraka zilizotolewa za maafikiano ya Marekani na Saddam Hussein kabla ya kuanzishwa vita dhidi ya Iran na kusema: Katika kipindi cha miaka yote ya vita hivyo nchi za Magharibi na Mashariki ziliendelea kuupatia misaada ya kijeshi, kiupelelezi na kifedha utawala wa Baathi wa Iraq kupitia nchi za Imarati, Saudi Arabia, Kuweit na njia nyingine.

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ametilia mkazo udharura wa kuwa macho mbele ya njama za adui za kutaka kupotosha ukweli kuhusu Vita vya Kujitetea Kutakatifu na kusema: Mfano mzuri wa rasilimali watu wa kipindi cha vita hivyo ni Shahidi Qassem Soleimani ambaye amefanya mengi ya kushangaza katika kanda hii na kwenye medani ya udiplomasia, na hadi sasa taifa la Iran halijajua ipasavyo huduma kubwa zizilitolewa na shahidi huyo azizi.
Kuhusu shughuli ya Arubaini ya Imam Hussein (as), Ayatullah Khamenei amesema kuwa, taifa la Iran linampenda na kumuashiki mjukuu huyo wa Mtume Muhammad (saw) lakini sula la matembezi ya Arubaini ya Imam linategemea maamuzi ya maafisa husika wa Tume ya Taifa ya Kupambana na Corona ambayo tayari imekataza matembezi hayo. Amewahimiza wananchi wote kufuata magizo ya tume hiyo.

3924250

captcha