IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
18:59 - October 21, 2020
News ID: 3473280
TEHRAN (IQNA) - Ukuras wa Twitter wa Kiongozi Maudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu umezungumzia hatua ya baadhi ya nchi za Kiarabu ya kutangaza uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Ujumbe huo umesema kuwa, mataifa ya Waislamu hayawezi kamwe kuvumilia udhalilishaji uliosababishwa na mapatano hayo.

Ukurasa huo wa Twitter wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu umeweka ujumbe huo usiku wa kuamkia leo Jumatano na kuongeza kuwa, utawala wowote ule utakaokaa kwenye meza ya mazungumzo na utawala ghasibu wa Kizayuni, basi utaitia hatarini heshima na itibari yake mbele ya watu wake.

Sehemu nyingine ya ujumbe huo imesema, kama Marekani inadhani kwamba itaweza kutatua suala la eneo hili kwa njia hiyo basi itambue inakosea sana.

Tarehe 15 Septemba 2020, mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE au Imarati) na Bahrain walijipelekea katika Ikulu ya Marekani White House na kutia saini mapatano ya kutangaza uhusiano wa kawaida na utawala pandikizi wa Kizayuni. Utiaji saini huo ulihudhuriwa pia na rais wa Marekani, Donald Trump na waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu.

Jana Jumanne na kwa mara ya kwanza, ujumbe rasmi wa UAE ambao ndani yake alikuwemo pia waziri wa uchumi wa nchi hiyo, Abdullah bin Touq, uliwasili katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ambazo zimepachikwa jina bandia la Israel kwa ajili ya kutia saini makubaliano mengine ya kujidhalilisha kwa Wazayuni.

3472894

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: