IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran

Wauaji wa Shahidi Luteni Jenerali Qassim Soleimani lazima walipiziwe kisasi

21:27 - December 16, 2020
Habari ID: 3473463
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, wauaji wa shahidi Luteni Jenerali Qassim Soleimani lazima walipiziwe kisasi na kisasi hiki hakina shaka na kitatekelezwa wakati wowote.

Wauaji wa Shahidi Luteni Jenerali Qassim Suleimani lazima walipiziwe kisasiAyatullah Sayyed Ali Khamenei amesema hayo leo mjini Tehran alipokutana na wajumbe wa Kamati ya Hauli ya Luteni Jenerali Qassim Soleimani aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) pamoja na familia ya shahidi huyo na kueleza kwamba, Shahidi Soleimani ni shujaa wa taifa la Iran na Umma wa Kiislamu.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, kwa kuzingatia kwamba, Shahidi Qassim Soleimani alikuwa mtu wa watu ili kufanya kumbukumbu na hauli yake pia kuna haja ya kutumiwa uwezo wa wananchi na juhudi za kiutamaduni zenye ubunifu.

Ayatullah Sayyed Ali Khamenei amesema kuwa, kuuawa Shahidi Luteni Jenerali Qassim Soleimani lilikuwa tukio chungu la kihistoria ambapo sambamba na kuashiria kubadilishwa shahidi huyo na kuwa shujaa wa taifa kwa ajili ya Wairani na shujaa wa Umma wa Kiislamu amesema kuwa, shahidi huyo mwenye daraja kubwa alikuwa mtu wa kimaanawi, ikhlasi na wa akhera na hakuna wakati ambao alikuwa akifanya mambo kwa kujionyesha.

Kadhalika Ayatullah Khamenei sanjari na kusema kuwa, Shahidi Qassim Soleimani aliushinda Ustikbari katika kipindi cha uhai wake na hata baada ya kuuawa kwake shahidi ameongeza kuwa, shughuli ya kusindikiza miili ya mashahidi Qassim Soleimani na Abu Mahdi al-Muhandis iliyohudhuriwa na mamilioni ya watu nchini Iran na Iraq iliwashangaza majenerali wa vita baridi vya Uistikbari na hicho kikawa kibao cha kwanza cha uso dhidi ya Wamarekani.

3941416

captcha