IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Wanaodai kutetea haki za binadamu waliunga mkono jinai za Saddam

20:15 - December 02, 2021
Habari ID: 3474631
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria jinai zilizofanywa na dikteta wa Iraq Saddam dhidi ya watu wa Iran na akasema: Saddam alikuwa akifanya jinai hizo kwa msukumo na uungaji mkono wa wanaojigamba kuwa watetezi wa haki za binadamu duniani.

Tovuti ya habari ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo imetoa matini ya hotuba aliyotoa Ayatullah Sayyid Ali Khamenei tarehe 21 Novemba katika mkutano na waandaaji wa kongamano la mashahidi 3,000 wa mkoa wa Ilam lililofanyika leo asubuhi.

Katika mkutano huo, Ayatullah Khamenei alisema, kuuawa shahidi wanamichezo na watazamji kadhaa wa mkoa wa Ilam katika shambulio la Februari 12, 1987 dhidi ya watu waliokuwa katika mechi ya soka kunakumbusha jinsi wanamichezo hao walivyouawa kidhulma; na sambamba na kukumbusha kuwa Saddam alifanya jinai hiyo kwa msukumo wa wanaojigamba kuwa watetezi wa haki za binadamu duniani alisema: waandishi na wasanii wabainishe na kuweka hadharani ukweli wa maafa hayo kimataifa ili kuwatambulisha na kuwafedhehesha watetezi warongo wa haki za binadamu.

Katika hotuba yake hiyo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alibainisha pia kuwa suala la shahidi na kufa shahidi ni tofauti na watu wanaouawa katika vita vilivyozoeleka duniani na akafafanua kwamba, mbali na shahidi na mpambanaji katika njia ya Mwenyezi Mungu kulinda mipaka ya kijiografia, analinda pia mipaka muhimu ya kimaanawi; yaani mipaka ya itikadi, akhlaqi, dini na utambulisho na kuitoa mhanga roho yake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kwa kutimizia ahadi aliyowekeana na Mola wake.

3476756

captcha