IQNA

Indhari kuhusu Ghaza kushindwa kukabiliana na COVID-19

22:19 - November 24, 2020
Habari ID: 3473389
TEHRAN (IQNA) - Shirika la Afya Duniani (WHO) limetahadharisha kuhusu janga la COVID-19 kusambaratisha mfumo wa afya katika eneo la Palestina la Ghaza, ambalo limezingirwa kinyama na Israel.

Abdulnasser Sobh Mkuu wa Ofisi ya WHO huko Ghaza ametahadharisha kuwa, kuongezeka kwa kasi idadi ya watu wanaoambukizwa corona au COVID-19 katika Ukanda wa Ghaza wiki iliyopita kumezidisha hali ya wasiwasi. Abdulnasser Sobh ameeleza kuwa, kuna uhaba wa suhula za kitiba katika Ukanda wa Ghaza na iwapo hali hiyo itaendelea kushuhudiwa katika eneo hilo mfumo wa afya utashindwa kukidhi mahitaji  kwa zaidi ya wiki mbili na hivyo kusambaratika.  

Mkuu wa Ofisi ya Shirika la Afya Duniani katika Ukanda wa Ghaza amesema kuwa shirika hilo limesaidia kuingizwa Ghaza suhula za kitiba zinazohitajika kwa ajili ya kukabiliana na maambukizi ya corona katika eneo hilo; na kwamba hatua kali za udhibiti zinapasa kuchukuliwa ili kukabiliana na corona na kupunguza idadi ya maambukizi miongoni mwa raia wa Palestina wanaoishi  Ghaza. 

Hadi sasa jumla ya watu 14,084 wamepatwa na corona katika Ukanda wa Ghaza huku idadi ya vifo ikiongezeka hadi 92.

Utawala dhalimu wa Israel ulililiweka eneo la Ukanda wa Ghaza chini ya mzingiro wa anga, nchi kavu na majini tangu mwaka 2006 na kusababisha masaibu na matatizo chungunzima kwa wakati wa Kipalestina wa eneo hilo. 

Mzingiro huo wa kinyama umesababisha eneo hilo kukumbwa na uhaba mkubwa wa dawa, chakula na mahitajio mengine muhimu.

3473195/

captcha