IQNA

19:41 - November 13, 2020
News ID: 3473356
TEHRAN (IQNA)- Makundi ya kutetea haki za binadamu yameutaka utawala wa Kizayuni wa Israel usitishe hujuma zake za kijeshi dhidi ya Ukanda wa Ghaza na uwalipe fidia wakulima uliowaharibia mashamba yao.

Taarifa ya pamoja iliyotolewa na Kituo cha Haki za Binadamu cha Al Mizan na Kituo cha Kisheria za Haki za Waarabu Israel, imetaka utawala haramu wa Israel usitishe mara moja  hujuma dhidi ya mashamba ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza.

Taarifa hiyo imesema mnamo Oktoba 13, 2020, mabuldoza ya jeshi la Israel yalivamia ardhi za kilimo za Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza na kuharibi mimea pamoja na mfumo wa usambazaji maji. Katika hujuma hiyo wakulima 10 walipata hasara ya zaidi ya dola 32,000.

Utawala wa Kizayuni hutumia visingizio mbali mbali kushambulia ukanda wa Ghaza angani na nchi kavu.

Tokea mwka 2006, utawala wa Kizayuni uliweka mzingiro katika Ukanda wa Ghaza kufuatia ushindi wa Hamas katika uchaguzi wa kidemokrasia. Mzingiro huo wa kinyama umesababisha eneo hilo kukumbwa na uhaba mkubwa wa dawa, chakula na mahitajio mengine muhimu.

3473100

Tags: ghaza ، palestina ، israel ، mashamba
Name:
Email:
* Comment:
* captcha: