IQNA

Aliyeuhujumu Msikiti na kuua Waislamu sita Canada apunguziwa adhabu

16:51 - November 27, 2020
Habari ID: 3473398
TEHRAN (IQNA)- Mtu ambaye alipatikana na hatia ya kuuhujumu msikiti na kuua Waislamu sita katika mkoa wa Quebec nchini Canada mwaka 2017 sasa anaweza kuwasilisha ombi la kuachiliwa huru baada ya miaka 25 gerezani.

Mahakama ya rufaa imetoa uamuzi huo na kudai kuwa hukumu ya mahakama ya chini dhidi ya Alexandre Bissonette ilikiuka katiba.

Mahakama ya Rufaa ya Quebec imesema huku ya awali ya kifungo cha maisha kwa Bissonnette  bila uwezekano wa kuomba kuachiliwa huru kwa muda wa miaka 40 ilikuwa kinyume cha katiba.

Waislamu sita – Aboubaker Thabti, Abdelkrim Hassane, Khaled Belkacemi, Mamadou Tanou Barry, Ibrahima Barry na Azzedine Soufiane – waliuawa wakati Bissonnette alipofyatua risasi ndani ya Kituo cha Kiislamu cha Quebec Januari 2017.

Hujuma hiyo ilijiri baada ya Swala ya Ishaa ambapo waumini wengi walijeruhiwa.

Msemaji wa Msikiti wa Quebec, Boufeldja Benabdallah, amesema wamesikitishwa na uamuzu wa mahakama ya rufaa. Amesema uadilifu haujatendekea na familia za waathirika zitaishi kwa uchungu.

Naye Yusuf Faqiri, mwakilishi wa Baraza la Kitaifa la Waislamu Canada amesema uamuzi wa mahakama ya rufaa ni dalili ya wazi ya undumakuwili.

3473237

captcha