IQNA

Wanawake Waislamu waliovaa Hijabu washambuliwa Canada

17:12 - February 06, 2021
Habari ID: 3473628
TEHRAN (IQNA)- Wanawake wawili Waislamu waliokuwa wamevaa hijabu walihujumiwa sehemu mbili tafauti Jumatano mjini Edmonton Canada.

Polisi ya Edmonton imehusisha hujuma hiyo na chuki dhidi ya Uislamu na kutangaza kuwa, Kitengo cha Jinai za Chuki na Misimamo Mikali kinachunguza hujuma hizo. Tukio hilo na katika msururu wa matukio kadhaa ya hivi karibuni Edmonton ambapo wanawake Waislamu wanaovaa Hijabu wamekuwa wakishambuliwa.

Katika tukio la kwanza mwanamke Mwislamu alishambuliwa katika eneo la University na mwingine katika eneo la Strathcona kusini mwa Edmonton.

Meya wa Edmonton Don Iveson amelaani hujuma hizo dhidi ya wanawake Waislamu na kusema hisia za chuki dhidi ya Uislamu hazina nafasi yoyote katika mji huo.

Kwa ujumla Canada ni nchi ambayo huwakaribisha wahamiaji na wafuasi wa dini zote lakini katika miaka ya hivi karibuni kumeshuhudiwa ongezeko la vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu.

Pamoja na hayo Waziri Mkuu Justin Trudeau amesema Waislamu nchini Canada wamekuwa na mchango mkubwa  nchini humo na hivyo hatua zitachukuliwa kwa wale wanaoeneza chuki dhidi ya Uislamu.

3952335

captcha