IQNA

TEHRAN (IQNA)- Qarii Yassri al Araq wa Iraq hivi karibuni alisoma aya za Qur’ani katika sherehe za kuadhimisha kuanzishwa Jeshi la Kujitolea la Wananchi maarufu kama al Hashd al Shaabi.

Alisoma aya za Sura al Tawbah katika halfa hiyo iliyofanyika mwishoni mwa mwezi Juni.

Harakati ya Al Hashd al Shaabi  iliundwa Juni 2014 kufuatia fatwa ya marjaa wa Iraq Ayatullah Sistani. Lengo la kuundwa harakati hiyo lilikuwa ni kupambana na kundi la kigaidi la ISIS au Daesh na kulinda mamlaka ya kujitawala Iraq. Kwa hivyo Al Hashd al Shaabi iliundwa kwa misingi ya kidini na kitaifa. Al Hashd al Shaabi  ilikuwa na nafasi muhimu sana katika kukabiliana na magaidi wa ISIS  nchini Iraq. Ni kwa kuzingatia nukta hiyo ndio  wakati alipokuwa waziri mkuu wa Iraq, Haidar al Ebadi mnamo 24 Februari 2016, wakati wa kukaribia kumalizika vita dhidi ya ISIS, alitoa amri kuwa Al Hashd al Shaabi ni taasisi ya kujitegemea ambayo itakuwa ikiendesha shughuli zake chini ya kamandi ya Majeshi ya Iraq.

Akihutubu katika mjumuiko huo wa kijeshi wa kuadhimisha kuanzishwa al Hashd al Shaabi, Waziri Mkuu wa Iraql Mustafa al Kadhimi alisema al-Hashd al-Shaabi ilifanikiwa kuangamiza magaidi wakufurushaji wa ISIS nchini humo.

 3982383