IQNA

Ndege za kivita za Marekani zahujumu mpaka Iraq na Syria

20:24 - February 26, 2021
Habari ID: 3473684
TEHRAN (IQNA)- Jeshi la Marekani kwa amri ya Rais Joe Biden limefanya mashambulizi ya anga yaliyolenga kambi za makundi ya muqawama yanayopambana na magenge ya kigaidi katika mpaka wa Iraq na Syria.

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon), John F. Kirby amesema Biden aliidhinisha kutekelezwa hujuma hizo za anga dhidi ya ngome za wanamuqawama wa harakati za kujitolea wananchi za Hashd al-Sha’abi, Kata'ib Hizbullah na Kata'ib Sayyid al-Shuhada mashariki mwa Syria.

Kirby amedai kuwa, Marekani imetekeleza hujuma hiyo kama jibu kwa mashambulizi ya hivi karibuni dhidi ya askari wa Marekani na waitifaki wao nchini Iraq.

Wanajeshi magaidi wa Marekani wako nchini Iraq tangu mwaka 2003. Mashinikizo yameongezeka ya kutaka wanajeshi hao vamizi watimuliwe nchini humo.

Kwa mujibu wa Pentagon, jeshi la Marekani limedondosha mabomu saba yenye uzani wa pauni 500 katika majengo yaliyoko katika mpaka wa Syria na Iraq.

Wadadisi wa mambo wanaitakidi kuwa, kumiminwa wanajeshi wa Marekani katika nchi za Syria na Iraq kwa madai ya kupambana na ugaidi, ni sehemu ya njama za wazi za Washington za kulifufua genge la kigaidi la Daesh (ISIS) ili ipate kuhalalisha uwepo wa wanajeshi wake katika nchi hizo.

3956322

captcha